Monday, 12 March 2018

NEW
Tokeo la picha la rosa ree
Hii video mpya ya Rosa Ree Ft Billnass ‘Marathon’ itazame hapa

Hii video mpya ya Rosa Ree Ft Billnass ‘Marathon’ itazame hapa

Read More

Saturday, 10 March 2018

Msanii wa HipHop asiyeishiwa na vituko kila uchao, Chid Benz amekiri kuuza nyumba yao ambayo iliyokuwa kwenye 'apartment' za ghorofa waliyokuwa wanaishi Ilala Jijini Dar es Salaam na kudai sio ya kwanza kuuza kwani ameshauza nyingi mpaka kufikia sasa
Tokeo la picha la Chid benz photos
Chid ametoa kauli hiyo kufatia mvutano mkali uliyobakia kidogo ampige ripota wa kipindi cha eNewz kutoka EATV, Duwe Santana baada ya kutaka kufahamu juu ya tetesi zilizokuwa zinazagaa kuwa rapa huyo ameuza ghorofa walilokuwa wanashea katika 'apartement' za Ilala na kupolekea kuishi kwa washkaji zake vichochoroni.
"Yeah mimi ndio nimeuza nyumba 'ghorofa' na siyo ya kwanza kuiuza nimeuza nyumba nyingi na sasa hivi naishi kwa Mama yangu mzazi ambapo nyumba nimejenga mimi. Hapa nina kwambia ni nyumba, nimezaliwa Ilala", amesema Chid Benz.
Mtazame hapa chini Chid Benz akitolea ufafanuzi juu ya kuuza nyumba yao ya Ilala Jijini Dar es Salaam.



Chid Benz auza mjengo wao Ilala

Read More

Ilikuwa siku ya kuzaliwa ya msanii Amber Lulu, Kupitia Sammisago.Com anafugnuka kwa mara ya kwanza kuhusu, UMRI Wake, Alivyojisomesha, Biashara alizofanya mpaka kufikia hapa,
Tokeo la picha la Amber Lulu photos
Mahusiano yake na Prezzo yameishia wapi, Picha ya TBT na Izzo Bizness,.

Amber Lulu Afunguka kuhusu UMRI Wake, Kuachana na Prezzoo, Ujauzito, Kufuta Tattoo ya Young Dee

Read More

Rapa Lil Wayne ana kesi ya kujibu baada ya mama mmoja aliyefahamika kama Keiotia Watson kuomba mahakama itoe amri kwa rapa Lil Wayne kupimwa DNA ili kupata ushahidi kuwa ni baba wa mtoto wake Dwayne mwenye umri wa miaka 15 .
Tokeo la picha la lil wayne 2018
Ikigundulika Wayne ni baba wa mtoto huyo, mama huyo atapokea dola 5000 kila mwezi na kulipwa fidia kwa muda wote aliomlea mtoto huyo bila baba.
Keiotia Watson anasema alikutana na Lil Wayne, aka Dwayne Carter,  June 2001 na kujifungua mtoto wa kiume February 2002.
Watson amekuwa akiomba vipimo hivi vifanyike kwa muda mrefu sasa na inaonekana mahakama iko upande wake.
Kama “Lil Dwayne” atakuwa mtoto wa Lil Wayne , huyu atakuwa mtoto wa tano wa rapa huyu.

Keiotia Watson kuomba mahakama itoe amri kwa rapa Lil Wayne kupimwa DNA

Read More

Baada ya Ester Ameruditena na hii AHSANTE unaweza kuitazama hapa 👇Usisahau KUSUBSCRIBE

Image may contain: 1 person, closeup

.

ITAZAME 👇

.


ITAZAME HAPA AHSANTE OFFICIAL MUSIC VIDEO BY DRAGON��

Read More

Friday, 29 December 2017



Itazame hapa video yanyimbo mpya ya Rayavanny Alomshirikisha Nikk wapili Tazama hapa 👇

Hii video mpya ya Rayvanny ft Nikk wa Pili - SIRI (Official Video)

Read More

Msanii wa muziki wa bendi kutoka Tanzania anaefahamika kwa jina la H.BABA Kupita ukurasawake wa instagram amepost picha ya Diamondplatnumz na Zariyhebosslady nakuandika maneno haya..


Mmetokelezeiyaa kinyama #Mmependezana #Mnaendana Allah Awasimamie #Ndoa Ifungwe Awe wako kwenye hesabu ya MWENYEZI MUNGU #Ntatoa #Ng'ombe (watano 5) wakubwa kabisa wakisukuma #waletwe #DAR #Huo ndio Uwezo wangu nahicho ndicho nitajaaliwa na MWENYEZI MUNGU #Nakutakia Maandalizi Mema ya NDOA Yako #Hongereni kwakupendana 👨‍👩‍👧‍👦👏👏 #MSIEMPENDA ATATOA NG'OMBE (watano)

Hechi baba alimalizia nakusema 👇
Naheshimu mahusiano ya #Mtanzania Mwenzangu #MIMI NIMZALENDO NIMEKATAA KUWA KAA #Usinilazimishe kwa maneno yako niwe #KAA
Narudia tena #NIMEKATAA KUWA #KAA 
#Watag kama umewajua #Mimi nawafahamu
#NG'OSHA NAKANDEKEJAA

MWAKA MPYA NAMAMBO MAPYAAAAAAAAAAAAAAA

@diamondplatnumz
@zarithebosslady

Mmetokelezeiyaa kinyama kama mtaowana ntatoa NG'OMBE WATANO(5):H.BABA

Read More

Msanii wa filamu Bongo na mwanamitindo, Jacqueline Wolper huenda akafunga ndoa hivi karibuni mara baada ya kuweka wazi mipango yake ya kwenda kumtambulisha mpenzi wake kwa wazazi wake.

Licha ya kutomtaja muhusika, Wolper ameeleza kuwa mpenzi wake huyo ameridhia suala hilo kwani naye pia alikuwa akilihitaji toka mwanzo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wolper ameandika mengi kuhusiana na hilo ila hapa tumenukuu haya machache;
Wewe ni mwanaume ambae umejitoa ili tu niwe wako,umetaka tufike mbali kwanza kabla ya mambo mengine (uwende kwa wazazi, (NDOA) pamoja na kwamba mahusiano yangu ya nyuma yalikuwa yana misukosuko mingi ila umemthamini Jacq. Nilipotoka niliteswa sana na mapenzi yaani usaliti, dharau, kukosa na mapenz ya dhati.
Pamoja ya kuwa pia alishatokea mmakonde na kunipeleka mapaka Mtwara na matembele nikachuma na wanakijiji kunipokea na kupikia familia na kutambulishwa kwa wazazi lakini sikufanikiwa kufikia hatua hii ambayo umefika, umenijali na umenisikiliza nilipokwambia sihitaji mtu bali nahitaji future husband.
Pia ameongeza kuwa katika mahusiano amejifunza kunyamaza bila kuyaweka hadharani na siku ya leo ndipo anatarajia kumtambulisha nyumbani kwao, Moshi na taratibu nyingine kama mahari kufuata.       
source-bongo5

Wewe ni mwanaume ambae umejitoa ili tu niwe wako:Jacqueline Wolper

Read More

Thursday, 28 December 2017

This file photo taken on November 18, 2017 shows supporters of Tajamuka Sesijikisile SA, The African Democrats Opposition Party, the Zimbabwe Communist Party, the Zimbabwe Diaspora Coalition and other groups attending a rally at the Union Buildings in Pretoria, South Africa, to call for the resignation of Zimbabwe"s President.
Matukio mengi ya kukumbukwa yalitokea mwaka 2017 yakiwemo kujiuzulu kwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na mabadiliko sambamba katika nchi za Gambia na Angola.
Isisahaulike kufutwa kwa uchaguzi wa rais nchini Kenya ,kitendo kilichofanyika kwa mara ya kwanza Afrika.
Pia tumeripoti kuhusu majanga na ubunifu - lakini hizi ni baadhi ya habari za kushangaza kwa mwaka 2017.

'Githeri Man'

Mwanaume mmoja Mkenya aliyepigwa picha akitafuna 'githeri' chakula cha mahindi na maharagwe, wakati wa uchaguzi, alijipatia umaarufu mkubwa.
'GitheriMan' akisimama kwenye foleni akishika mfuko wa plastiki
Githeriman, ambaye kwa jina lake halisi anaitwa Martin Kamotho, alivuma wakati wa uchaguzi mkuu wa Kenya tarehe nane mwezi wa nane alipoonekana kwenye mitandao ya kijamii akila chakula cha maharagwe na mahindi yakiwa ndani ya mfuko wake wa plastiki.
Bw Kamotho anajulikana sana kama "Githeri Man" alivuma sana kwenye mitandao ya jamii;
Makampuni makubwa kama vile Safaricom na Maisha Flour Milla yamejitokeza kumsaidia Githeriman na hivi sasa akaunti yake benki imeshiba kutokana na cheki alizoandikiwa na kampuni hizo.
Bw.Kamotho alikuwa miongoni ya wananchi 59 waliotunukiwa nishani za heshima na Rais Uhuru Kenyatta wakati wa sherehe za kuidhinisha sikukuu ya jamhuri kwa sababu ya kazi walioifanyia nchi.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, tuzo hiyo ni kwa minajili ya watu ambao "wameonesha uwezo wa hali ya juu, katika uongozi,ujasiri na uzalendo"
Hata hivyo baadhi ya Wakenya bado wanapata shida kufahamu ni nini hasa Bwana Kamotho alichofanya ili kupata heshima hiyo.

Dk. Shika wa milioni 900

Mnada wa nyumba za mfanyabiashara maarufu Said Lugumi,ulioharibika nchini Tanzania, iligeuka kumpatia umaarufu mwanaume mmoja kwa jina la Dk. Louis Shika .
Dk Shika alijizolea umaarufu baada ya kuibuka kwenye mnada huo na kutaja viwango vya juu vya fedha kuwapiku watu wengine waliojaribu kununua nyumba hizo.
Dk Shika aliwashangaza wengi kwa mavazi yake ya kawaida mbazo hazikumuonesha kama mtu ambaye angeweza nunua nyumba za dola za Marekani milion 15 (Sh bilioni 3.2)
Lakini baada ya kutolipa asilimia 25 ya fedha zilizohitajika, alikamatwa na polisi kwa shutuma za kuharibu mnada,na kuachiwa baada ya kulipa dhamana.
Kwa mujibu ya vyombo vya habari nchini humo, kauli zake katika mnada huo, hasa ya '900 itapendeza' ,ndizo zilizompa umaarufu kiasi cha kupata udhamini wa kampuni tofauti.
Baada ya hapo maswali mengi yalivuma kwenye mitandao ya kijamii, kuhusu ukweli wa hali yake Dk Shika,ambazo zinadai kwamba alikuwa mjasusi wa intelijinsia wa Marekani, CIA, anamiliki mabilioni ya fedha nchini Urusi na Uhispania.

"Polisi Kinyozi" aliyewaibisha wanawake

Mwezi Aprili, taasisi ya usalama barabarani Nigeria, walimuadhibu kamanda aliyepigwa video akiwaadhibu wafanyakazi wa kike kwa kuwakata nywele zao ndefu.
Picha zilimuonesha komanda huyo akitumia mkasi kuwakata nywele wakati wa ukaguzi na kuzua hisia za hasira mtandaoni.
Inasemekana kuwa wanawake hao walikuwa wamevunja kanuni za mitindo za nywele inayoruhusiwa na taasisi ya usalama barabarani (FRSC)Mwanaume mwenye kofia nyekundu akimkata nywele mwanamke hadharani
Msemaji wa FRSC alisema kitendo cha afisa huyo kilikuwa nje ya udhamini wa taasisi hiyo.
Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa jamii wa Twitter , Lauretta Onochie, msaidizi wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, alikemea kitendo hicho na kukiita "udhalilishaji wa wanawake"

Kanisa la Walevi

Kanisa jipya nchini Afrika ya Kusini lilifungua milango yao na kuwakaribisha wavuta sigara na wanywaji pombe , ambao kwa kawaida hawapatiwi nafasi katika makanisa ya walokole.
Mtandao wa Habari Afrika Kusini ya eNCA, iliripoti kuwa, kanisa la Gobola mjini Johannesburg liliwakaribisha makundi ya watu na chupa za bia wakati wa ibada.
Askofu wa kanisa hilo, Tsietsi Matiki alisema kanisa ni "sehemu mwafaka" kwa wanywaji pombe na wavutaji sigara.
Lakini, eNCA wanaeleza , baraza la makanisa Afrika Kusini limelipinga kanisa hilo mpya.
Kwa mujibu wa mshiriki mmoja wa kanisa la Gobola, pombe inapewa tu kwa waumini waliona umri wa miaka 20 kwenda juu.
Mwanaume mwenye upara

Vipara Msumbiji Walengwa

Mwezi Juni , polisi nchini Msumbiji walionya kuwa wanaume wenye vipara huenda wakalengwa kwenye mashambulizi yanayohusiana na uchawi.
Watu wanaamini kwamba mwili wa mtu mwenye kipara una dhahabu , kulingana na kamanda mmoja wa polisi kwa jina Afonso Dias aliiambia BBC mnamo mwezi Juni baada ya misururu ya mauaji yaliyolenga watu wenye vipara.
Watu watano waliuwauwa wakati tuliporipoti habri hiyo.
Polisi pia waliwakamata watuhumiwa wawili walioshiriki katika mauaji hayo ya uchawi.
Soma zaidi hapa na hapa

Wabunge watwangana makonde Uganda

Wabunge nchini Uganda walipigana ndani ya ukumbi wa bunge wakiwa katika kikao cha kujadili wa muswada wa kuondoa ukomo wa miaka ya kugombea nafasi ya urais kwa mjibu wa katiba ya taifa hilo
Wabunge wa upinzani wanadai kuwa kama kikomo cha umri wa miaka 75 kitaondolewa ni njama za kumuandilia njia Rais Yowei Museveni, mwenye miaka 73, kugombea tena mwaka 2021.
Katika kanuni za Katiba, mtu anayewania urais haruhusiwi kuwa na umri zaidi ya miaka 75.
Wanawake wa Sudan wakiwa Khartoum

Suruali ni Marufuku Sudan

Polisi nchini Sudan walivamia sherehe katika mji mkuu wa Khartoum mwezi Disemba na kuwakuta wanawake wakivaa suruali.
Wanawake 24 walikamatwa na kushtakiwa kwa kutokuwa na maadili lakini baadaye mashtaka hayo yalifutwa.
Shambulio hiyo ilifanywa na idara ya poilisi yenye mamlaka ya kulinda maadili.
Kama wanawake hao wangehukumiwa, wangepata adhabu ya mijeledi 40 na kutozwa faini.
Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa maelfu ya wanawake wanakamtwa na kupigwa kwa "kuvaa nguo zisizo na maadili" kila mwaka na kuichapwa mijeledi.
Wanasema sheria inayopiga marufuku kuvaa suruali, sketi fupi au ya kubana katika nchi ambayo wengi ni Waislamu, ni ubaguzi dhidi ya Wakristo.
Kitamaduni, wanawake wa Sudan wanavaa nguo ndefu zisizobana kama baibui.

#WengerOut

Maneja wa timu ya Arsenal ya Uingereza, Arsene Wenge anaendelea kuwagawana mashabiki wa klabu ya Arsenal, barani Afrika na kwengineko.
Mwezi Novemba, wakati Wazimbabwe wengi walikuwa wanatafakari kuhusu jeshi kuchukua mamlaka na maandamano katika mji mkuu wa Harare yaliotaka kumtoa Robert Mugabe mamlakani, wengineyo walichukua muda wao kudai Wenger aachie madaraka.

Habari: Zilizo Kiki Afrika 2017

Read More

Msanii wa muziki wa bongo fleva Harmorapa amefunguka na kumuomba radhi mtayarishaji mkongwe wa muziki wa bongo fleva na mmiliki wa studio za Mj Records, Master J na kusema kuwa amegundua kuwa alimkosea mkongwe huyo kwenye muziki.

Harmorapa alifunguka hayo alipohojiwa kwenye kipindi cha eNewz cha EATV na kusema katika mwaka 2017 amekosea sana Master J kufuatia kauli yake aliyoitoa kipindi cha nyuma kupitia kipindi hicho kuwa hamjui wala hamtambua mtayarishaji huyo mkongwe wa bongo fleva. 
"Nimegundua kuwa nilifanya makosa sana, unajua kipindi kile nasema vile nilikuwa bado sijamjua vizuri Master J hivyo naomba anisamehe tu kwani ulikuwa ugeni katika tasnia hivyo nilikuwa sijamjua vizuri" alisikika Harmorapa.

Nimegundua kuwa nilifanya makosa sana, nilikuwa bado sijamjua vizuri Master J

Read More

Tuesday, 26 December 2017

Tokeo la picha la joh makini mipaka

itazame hapa

Itazame hapa Video mpya ya Joh makini #MiPAKA (Official Video)

Read More

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Nairobi Kenya baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana, ameanza kusimama kwa mara ya kwanza kwa msaada wa madaktari.

Taarifa kutoka Hospitali ya Nairobi imeeleza kuwa Lissu kwa mara ya kwanza ameweza kusimama kwa msaada wa Physiotherapist tangu  Septemba 7, mwaka huu alipopigwa risasi mjini Dodoma, hatua chache kabla ya kufika nyumbani kwake.
Akizungumza kutoka Hospitalini hapo, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanansheria Tanganyika (TLS), amesema "Wapendwa wote wiki iliyopita niliwataarifu kwamba  madaktari wangu wamesema nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania"
"Leo Boxing Day nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa mababa cheza kama inavyoonekana, hatua inayofuata nitawajulisheni," Lissu

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu kusimama kwa mara ya kwanza

Read More

Monday, 25 December 2017

Harmorapa amefunguka na kusema kuwa katika mwaka 2017 amehangaika kulipata penzi la mwanadada Wema Sepetu kiasi cha kuamua kwenda kwa mganga wa kienyeji mara tatu ili aweze kumpata mrembo huyo.
Tokeo la picha la wema sepetu na hamorapa
Harmorapa akipiga stori kwenye kipindi cha eNewz cha EATV amedai kuwa baada ya kuhangaika kwa marafiki zake Wema Sepetu na kugonga mwamba aliamua kwenda kwa babu (mganga) ambapo amedai kwa mara ya kwanza aliambiwa apeleke kuku mweupe, na alipeleka huyo kuku lakini aliporudi mjini Dar es Salaam mambo yake yakawa bado vile vile.
"Nimemuendea kwa babu Wema Sepetu mara tatu, nilipokwenda mara ya kwanza niliambiwa nipeleke kuku mweupe, nikapeleka zangu yule kuku mganga akafanya yake lakini niliporudi mjini sikuona mabadiliko yoyote yale, nikamfuata tena babu akaniambia nipeleke vitu vingine viwili ambavyo hapa nashindwa kuvisema" alisema Harmorapa 
Harmorapa aliendelea kufunguka jinsi ambavyo amehangaika na kulitafuta penzi la Wema Sepetu na kudai ilifika wakati aliambiwa apeleke mchanga wa unyayo wa Wema Sepetu au mchanga ambao mwanadada huyo ametemea mate, kitu ambacho Harmorapa amedai kilikuwa kigumu sana kwake kwa sababu hapati nafasi ya kukutana live  Wema Sepetu.
Hata hivyo Harmorapa kwa sasa amesema amemwachia Mungu juu ya jambo hilo baada ya kuona harakati za kwa mganga wa kienyeji zinakwama. 

Nimemuendea kwa babu Wema Sepetu mara tatu.

Read More

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top