Akifanya mahojiano na kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na East Africa Television, na kusema kwamba hajazaa na binti huyo na wala hajawahi kukutana naye kimwili.
Licha ya kuchezwa sauti ya binti huyo ikiongolea kuwa Baraka ndiye baba wa mtoto huyo, amesema ingawa mama mtoto kasema ni wake lakini sio kauli ya kuamini kwani ameshapitia mambo kama hayo.
“Nina mtoto mmoja yuko Arusha, mama anaitwa Farida, ni mtoto wangu, hizo stori zingine sio kweli”, amesema Baraka The Prince.
Pamoja na hayo Baraka amekanusha taarifa za kuachana na mpenzi wake, na kusema kwamba bado wapo pamoja.
0 comments:
Post a Comment