Monday, 19 June 2017

Ben Pol 'Tatu' video ya wimbo wake mpya ‘Tatu’ aliomshirikisha Darassa haijatoka.

Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol ameeleza ni kwanini hadi sasa video ya wimbo wake mpya ‘Tatu’ aliomshirikisha Darassa haijatoka.

Ben Pol
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Show Time cha Radio Free Africa, kuwa hawakutaka kutoa video ya wimbo huo kipindi cha Mfungo wa Ramadhan, ingawa hadi sasa imeshakamilika.
“Video ya tatu imeshaisha na tayari ninayo, video imeshashutiwa na nipo nayo hapa ndani zaidi ya wiki moja na nusu sasa, naiangalia naonesha na watu, Sema tu kwenye time ndio tunaangalia tutoa muda gani kwa sababu hatukutaka kutoa kati kati ya Ramadhani, kwa hiyo mwishoni mwa mwezi wa Ramadhan itatoka,” amesema Ben Pol.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top