Thursday, 23 November 2017

HIZI NDIZO TIMU ZILIZOFUZU HATUA YA MTOANO UEFA NA ZILE ZINAZOENDA KUSHIRIKI EUROPA

Tokeo la picha la ronaldo 7

UEFA Champions league imeendelea tena siku ya jana kwa Michezo ya mzunguko wa tano hatua ya Makundi huku Vilabu mbalimbali vikipata nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora huku klabu zingine zikihitajika kushinda Michezo yao ya Mwisho ili kujihakikishia kufuzu au kutupwa katika Michuano ya Europa na zingine kutolewa kabisa.

Katika Kundi A Klabu ya Manchester United ina nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya 16 bora ingawa inahitaji ushindi katika Mchezo wa Mwisho dhidi ya CSKA ili imalize nafasi ya kwanza katika kundi hilo baada ya kupoteza Mchezo siku ya jana dhidi ya FC Basel. United itashindwa kufuzu ingawa itafungwa Mchezpo wake wa mwisho kwa zaidi ya Magoli 6. CSKA pamoja na Basel zote zina nafasi ya kufuzu hatua ya 16 kama zitashinda michezo yao ya mwisho huku zote zikiwa na alama 9 mpaka sasa.

Kundi B tayari Klabu ya PSG pamoja na Bayern Munich zimefuzu hatua ya 16 bora huku PSG ikiweka historia ya kufuzu hatua ya makundi kwa kufunga magoli mengi (Magoli 24), klabu ya Celtic pamoja na anderlecht zinagombania nafasi ya kushiriki Europa.

wenye Kundi C klabu ya Chelsea imefuzu tayari, Roma itahitaji kushinda dhidi ya Qarabang ili iweze kumaliza nafasi ya kwanza kama Chelsea atapoteza dhidi ya Atletico Madrid katika Mechi ya mwisho. Roma na Atletico wote wana nafasi ya kufuzu ingawa Qarabang hawezi kufuzu hata akishinda Mchezo wa mwisho kwa idadi yoyote ya Magoli.

katika kundi D Barcelona pekee ndiyo klabu ambayo imeshafuzu hatua ya 16 bora huku klabu ya Juventus,Sporting Lisbon zina nafasi ya kufuzu pia Olympiakos haiwezi kufuzu hata ikipata ushindi katika Mchezo wa mwsiho

Picha inayohusiana
Katika Makundi mengine Real Madrid na Tottenham wamefuzu katika kundi H, Manchester City imekata tiketi tayari ya kucheza hatua ya mtoano katika kundi F huku Besiktas wakifuzu pia katika kundi G.

Mpaka sasa timu zote tano zina nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya 16 bora huku timu za Ujerumani mpaka sasa Borrusia Dortmund ikiwa tayari imetolewa katika Michuano hiyo na itaenda kushiriki michuano ya Europa. Michezo ya mwisho ya makundi itaendelea tena Desemba 5.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top