Tuesday, 5 September 2017

Alexander Graham Bell Mfahamu leo na lambegu0416

Mfahamu Alexander Graham Bell leo na lambegu0416 

Mtu wa kwanza kugundua simu aliitwa Alexander Graham Bell mwaka 1876. Huyu jamaa alikuwa na mpenzi wake aitwaye Mabel Margaret Hello ambaye alimuoa mwaka 1877. Kipindi cha nyuma alipokuwa akimpigia simu mpenzi wake, kitu cha kwanza kabisa alichokuwa akikifanya ni kumuita jina lake ‘Hello’ halafu mpenzi wake anaitikia.

Alexander Graham Bell (3 Machi 1847 – 2 Agosti 1922) alikuwa kati ya wagunduzi wa mawasiliano ya simu. Alizaliwa katika mji wa Edinburgh nchini Uskoti lakini baadaye alihamia nchi za Kanada na Marekani. Baba yake alikuwa mwalimu wa watoto wenye matatizo ya kusikia na kuongea.

 Alifanikiwa katika jaribio lake la kwanza mwaka 1876.
Bell hakuwa mtu wa kwanza wa kutengeneza simu kwa mawasiliano lakini mashine yake ilikuwa ya kwanza iliyoweza kutumiwa kibiashara nje ya majaribio na maabara. Alitumia matokeo ya utafiti wa watangulizi hasa Mwitalia Antonio Meucci.


Linakuwa si jambo kubwa kumsahau aliyegundua simu, ila afadhali kidogo unaweza kumkumbuka mpenzi wake na kumuita kila unapopigiwa au unapopiga simu.
Alexander Graham Bell akiwa na mpienzi wake Mabel Margaret Hello

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top