Tuesday, 20 June 2017

Confederation Cup 2017:Bila Mesut Özil wala Thomas Müller mambo safi

Jumatatu hii umechezwa mchezo mmoja wa kumalizia mzunguko wa kwanza wa kombe la mabara kwa ngazi za timu za taifa (Confederation Cup) nchini Urusi ambapo Australia walikuwa wakicheza na Ujerumani.


Katika mchezo huo Ujerumani waliibuka wababe kwa ushindi wa mabao 3-2.
Magoli ya Ujeumani yalifungwa na Lars Stindl (43), Julian Draxler (48) na Leon Goretzka (57) na magoli ya Australia yalifungwa na Lars Stindl (4), Tom Rogic (41).
Kwa sasa mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani ni ile itakayowakutanisha Ujerumani dhidi ya Chile siku ya Alhamisi hii huku Australia wakicheza na Cameroon.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top