Saturday, 17 June 2017
Rais wa Visiwa vya Vanuatu afariki dunia
Vanuatu. Rais wa visiwa vya Vanuatu, Baldwin Lonsdale amefariki dunia kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni mshtuko wa moyo leo.
Lonsdale ambaye pia ni Kasisi wa Anglikana amekuwa kiongozi wa kisiwa hicho cha Pacific
kwa miaka miwili tangu Septemba 2014.
Gazeti la Daily Post nchini Vanuatu limesema kuwa Lonsdale alifariki ghafla kwenye mji
mkuu wa Port Vila usiku wa kuamkia leo.
Akiwa rais, Lonsdale aliongoza ujenzi mpya wa maeneo ya kisiwa hicho kufuatia uharibifu
uliosababishwa na kimbunga cha Pam kilichosababisha watu 75,000 kukosa makazi mwezi
Machi mwaka 2015.
Oktoba mwaka huohuo aliapa kupambana na ufisadi nchini humo baada ya sakata
lililomhusisha makamu wake la matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

0 comments:
Post a Comment