Monday, 19 June 2017

Zijue njia sahihi za kuweza kutimiza malengo yako


Leo nitaongelea swala la kutimiza malengo yako ndani ya wakati hasa kwa vijana ambao katika ujana tunakua na mambo mengi sana ya ujana hadi kusababisha kufeli kwa malengo yetu.... Sasa ni Njia zipi hasa uzifate ili malengo yako yaweze kutimia kama ulivopanga?
 unafanya kazi kwa bidii kila siku lakini hutimizi lengo ulilo panga? Je, unakosea wapi mbona huwezi kukamilisha malengo yako kwa wakati?
Karibu twende sawa....

Kwa Kawaida  kila binadamu akishaanza kupevuka anakuwa na malengo yake ambayo anatamani kuyatimiza tena ikibidi hata kwa mara moja..... ila hakuna mtu anaeweza kutimiza malengo yake ya sasa na baadae kwa wakati mmoja hivyo lazima uweke mikakati ambayo itakusaidia kutimiza malengo yako ya sasa na baadae

Kwa mwaka huu 2017 kila mtu ameweka malengo yake ya kutimiza, na kila mtu anatamani inapofika mwisho wa mwaka awe ametimiza malengo hayo ni  wachache sana hutimiza malengo yao, lakini wengi hushindwa kutimiza  na bila kujiuliza  kwanini malengo uliyojiwekea hayajatimia..na bila kujua  ulikosea wapi badala yake  tuna weka malengo mengine mapya ya kitimiza mwaka unaofata na kisahau lengo ambalo hujalitimiza lina umuhimu kiasi gani kwenye maisha yako kama kijana na mwaka unaofata kosa linakua lile lile

Mtu mmoja ajulikanae kwa jina la LEO BABAUTA huyu ni mwandishi wa habari na vitabu na pia mmiliki wa blog moja inayojulikana kwa jina la Zen Habits aliliona tatizo hili kwa watu wengi hvyo aliamua kuongelea njia za kukamilisha malengo yako kwa usahihi na ndani ya muda uliopanga.. Aliziongelea njia saba mimi nitazitaja hapa halafu Mungu akijaalia nitaanza kuzielezea moja baada ya nyingine.

1:Chunguza malengo yako
2:Anza taratibu
3: Chagua lengo moja
4: Liweke lengo lako hadharani
5: Lifurahie lengo lako
6:  Chapisha lengo lako
7:  Jenga matarajio




By Jay Speed

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top