Wayne Rooney mapema leo akimwaga wino
Kupitia mtandao wa Klabu ya Everton taarifa zimesema wamefikia
makubaliano hayo kwa mazungumzo ya muda mrefu na baada ya kutathmini
uwezo wake na umri pamoja na uzalendo wake kwa klabu hiyo ambayo ndiyo
imemkuza tangia akiwa na mika nane kabla ya kununuliwa na Man united
mwaka 2004.Dili la Manchester United kumchukua mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku limehusishwa pia na usajili wa nahodha huyo kipenzi cha mashabiki wa Man united, Wayne Rooney .
Tayari Rooney amekubali kujiunga na Everton kwa kupunguza mshahara wake wa wiki kutoka paundi 250,000 anazolipwa sasa na Manchester United mpaka 180,000 kiasi ambacho Everton wamekiri kukimudu.
Rooney kukubali kujiunga na Everton ni kujipatia tiketi ya kutembelea Tanzania kuja kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia alhamisi ya wiki lijalo (tarehe 13 julai).
Hii itakuwa fursa pekee kwa watanzania kumshuhudia nahodha huyo wa muda mrefu wa timu ya taifa ya England na klabu ya Manchester United kutua kwa mara ya kwanza nchini Tanzania

0 comments:
Post a Comment