Thursday, 27 July 2017

Justin Bieber amekuwa akiandamwa na matatizo ni baada ya kukatazwa kufanya tamasha lake nchini China.

Siku ya jana msanii huyo alijikuta akimgonga na gari mpiga picha mwenye miaka 57 baada ya kutoka kanisani. Tukio hilo limetokea maeneo ya Beverly Hills nchini Marekani.
    Justin Bieber  alijikuta akipatwa na hofu baada ya kumgonga kwa bahati mbaya mtu huyo hali iliyopelekea kutoka katika gari na kumuhoji aliyemgonga anataka nini ili aondoke eneo la tukio.
Hata hivyo dakika chache Polisi wa Sgt. Matthew Stout waliwasili eneo la tukio na kumsaidia msanii huyo kutoa msaada kwa majeruhi ambaye alikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu baada ya kupata majeraha.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top