Wednesday, 12 July 2017

Tujifunze na kujisifu kwa kuwa na King Alikiba maana anautendea haki mziki wetu wa bongo fleva

Harmorapa, amefunguka na kusema Alikiba ni msanii ambaye amekosa mfano hapa Tanzania kutokana kazi zake na namna ambavyo amekuwa akifanya mambo yake nje ya muziki. 
"Katika vitu ambavyo tunatakiwa kujivunia ni kuwa na wasanii ambao wanatangaza taifa letu mbele na kujivunia juhudi zao. Naimani heshima, busara na juhudi ndiyo nyenzo pekee zilizowafanya wazungu kumwaga wino na kumkaribisha Alikiba meza moja na kumkabidhi kampuni kubwa ya Rockstar4000 kuwa mmiliki mmoja wapo na Director" alisema Harmorapa 
Mbali na hapo Harmorapa aliwataka wasanii wengine kujifunza na kujivunia uwepo wa Alikiba kwani amekuwa akiutendea haki muziki wa bongofleva na kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania nje ya nchi.
"Wasanii wa Tanzania inabidi tujifunze na kujisifu kwa kuwa na King Alikiba maana anautendea haki mziki wetu wa bongo fleva, hongera zangu zizidi kutiririka kwa King wewe uliokosa mfano hapa bongo" alisisitiza Harmorapa

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top