Thursday, 7 September 2017

Wema sepetu alia kuhusu tukio la kupigwa risasi Tundu lisu.

Tukio lililotokea mchana wa Alhamisi hii kwa kupigwa risasi kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu limewaumiza watu wengi ndani na nje ya Tanzania, miongni mwao ni malkia wa filsamu nchini Wema Sepetu.
Mrembo huyo atakuwa anaumia zaidi kuliko hata watu wengine kutokana na ukaribu wake na Mbunge huyo ambaye wote kwa pamoja wanakitumikia chama cha Chadema na kubwa zaidi ni wakili wake anayesimamia kesi ya madawa ya kulevya inayomkabili muigizaji huyo.

Kupitia mtandao wa Instagram, Wema ameandika:


Kwanza wamuhangaishe kila kukicha kesi haziishi… Akisema kitu uchochezi, sasa kakataa kukaa kimya ndo wameona wamuue…. NO!!! Watanzania kama tutaendelea kufumbia macho huu uonevu then hatutofika tunapotaka… Kero zinazidi kila kukicha… Ndugu zetu wanaonewa kila kukicha… And wat do we do…? Tunakaa Kimya… Jamani kwa hili tuombe tu Mungu huyu baba apone… Nikimaanisha, huko alipo sasa Mungu amsimamie na arudi kwenye hali yake…. Hii sasa imekuwa too much… This is something No One Can Take… Sidhani kama kuna Mtanzania yoyote anaependa hali ya nchi inavyoendelea kuwa kadri siku zinavyozidi kwenda… Ni nini hiki jamani…??? Oh Lord help my Uncle… If anything happens to him then nadhani wengi wetu vitatutokea maana hatutokaa KIMYA…!!! Ni kutokukaa kimya ndo kumepelekea haya yote kutokea… Nimeikumbuka Tanzania yetu ya miaka kama miwili iliopita… Sio Tanzania hii isio na Amani…

.
.
.
by bongo5

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top