Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari -Maelezo uliopo jijini Dar es salaam, Dk. Shika amesema ” Ninatarajia usiku wa 900 inapendeza nitaongea na wakazi wa Dar es salaam tutazungumza mengi, nawaomba mjitokeze na nimejiandaa vyema. Mkifika nyote itapendeza zaidi,” amesema Dk. Shika.
Aidha Dk. Shika amesema kuwa katika huo atazungumza mengi kuhusu maisha yake na kuwapa vijana hamasa kuhusu mambo ya ujasiliamali.
Hafla hiyo itafanyika tarehe 9 Disemba mwaka huu katika ukumbi Ukumbi wa Dar live huku akisindikizwa na burudani mbalimbali kutoka kwenye bendi ya Twanga Pepeta, Jahazi Modern Taarabu na mchekeshaji maarufu Emmanuel Mathias (Mc Pilipili)atahudhuria usiku huo.
JIUNGE NA BONGO5.COM SASA
0 comments:
Post a Comment