Abbas Suleiman Mratibu wa Simba SC, Amesema kuwa timu hiyo imesafiri kwaajili ya kupeleka burudani kwa wakazi wa mkoa huo ambako itacheza mechi moja kesho ili mashabiki wapate kuishuhudia timu yao.
“Timu imeenda Katavi leo kwaajili ya mechi ya kirafiki ya kuwapa burudani mashabiki wetu wa Katavi siku ya kesho na baada ya mchezo huo timu itarejea Mbeya kuendelea na kambi ya maandalizi ya mchezo wetu na Prisons”, amesema Abbas.
Simba itacheza na Tanzania Prisons Novemba 18 ukiwa ni mchezo wa raundi ya 10 lakini kabla ya mchezo huo klabu hiyo inaweza kwenda wilayani Kyela kucheza mechi ya kirafiki endapo benchi la Ufundi litaafiki kuwepo kwa mchezo huo.
Simba SC jana ilishinda 1-0 kwenye mchezo wake wa raundi ya 9 dhidi ya Mbeya City na kurudi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara. Ligi itasimama kwa wiki mbili kupisha kalenda ya mechi za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ambapo Tanzania itacheza na Benin ugenini.
0 comments:
Post a Comment