Addo Shaibu ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba licha sasa hivi ACT Wazalendo kimeamua kuendeshwa kiharakati kama ilivyo CHADEMA, na licha ya kutaka kuunganisha nguvu katika baadhi ya mambo ambayo yataupa ushindi upinzani, lakini ifahamike kuwa hana mpango wa kurudi huko.
“Tunajua kwa nini Zitto aliondoka, alikuwa na mgogoro na CHADEMA, na ndio sababu ya kuanzisha ACT, wakitazama lugha yake kwamba wapinzane tushirikiane wanaona kama lugha yake na CHADEMA imekuwa haina tofauti, mazingira ya kisiasa ndio yanalazimika hivyo, mambo wanayoyapitia CHADEMA na sisi tunayapitia, inalazimisha lugha iwe ya pamoja, hatuwezi kuunganisha vyama, na nakuhakikishia Zitto hana mpango kwa sasa wa kurudi ndani ya CHADEMA”, amesema Addo Shaibu.
Hivi karibuni Zitto Kabwe alisikika akiomba ushirikiano kutoka kwa vyama vya upinzani hususan CHADEMA ili kuweza ksuhinda kwenye chaguzi ndogo ndogo za udiwani zinazokuja, na kuibua hisia kuwa huenda chama hicho sasa kinataka kujiunga na CHADEMA kuwa pamoja.
0 comments:
Post a Comment