Friday, 1 December 2017

100,000 nchini Bangladesh walifurika katika uwanja wa wazi mjini Dhaka wakimshangilia Papa Francis.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Ijumaa ameongoza misa ya wazi katika mji mkuu wa Bangladesh Dhaka kabla ya kukutana na wakimbizi wa jamii ya Rohingya walioko nchini humo ambalo ndilo suala lililochukua uzito wa juu katika ziara yake nchini Myanmar na Bangladesh.
Image may contain: 2 people, people standing
Kiasi ya waumini wa kanisa Katoliki 100,000 nchini Bangladesh walifurika katika uwanja wa wazi mjini Dhaka wakimshangilia Papa Francis wakati alipokuwa katika eneo hilo akiwa ndani ya gari la wazi lililoandaliwa maalumu kwa ajili ya hafla hiyo. Muda mfupi baada ya kuwasili kutoka nchi jirani ya Myanmar Kiongozi huyo mkuu wa kanisa Katoliki duniani ametoa mwito kwa ulimwengu kuchukua hatua katika kutafuta suluhu ya mgogoro ambao umepelekea zaidi ya waislamu 620,000 wa jamiii ya Rohingya kukimbilia nchini Bangladesh.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top