Rais John Pombe Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali wakipata picha ya pamoja na bendi ya Mrisho Mpoto
Katika uzinduzi huo msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto akiwa pamoja bendi yake, Mpoto Band alitoa burudani ya aina yake na kuwavutia viongozi wa serikali waliojitokeza katika uzinduzi huo.
Baada ya uzinduzi huo kumalizika, muimbaji huyo aliitwa na Rais John Pombe Magufuli kwaajili ya picha ya pamoja ambapo pia akipata fursa ya kuzungumza na rais mambo kadhaa kuhusu muziki wake.
Akiongea na mwandishi wetu muda mchache baada ya picha hizo, Mpoto alisema bado rais anairudia kauli yake ya kusema kwamba anaupenda sana muziki wake na achoki kuusikiliza.
“Ni kweli niliitwa nikapiga naye picha baada ya hapo akawa anasema anaupenda sana muziki wangu, anaisikiliza sana Sizonje,” alisema Mpoto.
Aliongeza, “Mimi binafsi hiyo kauli yake sio mara ya kwanza kuisema, amekuwa akiirudia mara kwa mara na imenifanya nifikirie vitu ngingi sana, unajua kuandaa wimbo ambao utamfanya rais wa nchi kila akikaa auzungumzie ni kitu kikubwa sana na jambo ambalo linanifanya nione nimefanya kazi kubwa sana na pia namshukuru kwa kuendelea kuusikiliza muziki wangu kwa sababu kama unavyojua wasanii ni wengi sana, rais akipata fursa ya kuzikiliza nyimbo yako kila mara ni jambo la heri sana,”
Angalia picha za uzinduzi wa mradi huo.
source BONGO5
0 comments:
Post a Comment