uwekaji jiwe la msingi katika ofisi za Takwimu Taifa mjini Dodoma, na kusema kwamba watu wanaosema vyuma vimekaza hawako sahihi juu ya hayo, kwani uchumi wa nchi uko sehemu nzuri, na kwa kuwa walizoea kupiga hela za serikali.
“Ninawaomba Watanzania mpuuze uzushi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwamba uchumi umeshuka. wanaosema vyuma vimebana, vitabana tu kwa wale waliokuwa wamezoea fedha za bure bure, na vitaedelea kubana kweli kweli Lakini kwa wale wanaochapa kazi, kwa mfano wakazi wa Lindi na Mtwara, walikuwa wanauza korosho saa nyingine kwa bei ya chini mpaka elfu 2 kwa kilo, sasa elfu 4 kwa kilo. Wale vyuma haviwezi vikabana, wale vyuma vimeachia, nasikia wanaamua hata mbuzi kuzinywesha bia, kule vyuma vimefungua., hivyo wapuuzieni watu wanaowadanganya vyuma vimekaza”, amesema Rais Magufuli.
Pamoja na hayo Rais Magufuli amewataka wananchi kupuuzia watu wanaotoa takwimu za uongo, na kusema kwamba wenye mamlaka ya kutoa takwimu za taifa ni ofisi ya Taifa ya Takwimu pekee
source-EATV
0 comments:
Post a Comment