Saturday, 23 December 2017

Sylvester Stallone Aka Rambo kuhusishwa na Skendo ya Ubakaji

Mwanamke aliyedai kufanyiwa matendo ya ubakaji na mwigizaji mkongwe Sylvester Stallone Aka Rambo miaka ya tisini aomba kesi kufunguliwa upya na uchunguzi kufanyika ata baada ya muda wa kutoa mashtaka ya kosa hilo kupita.

Picha inayohusiana

Dada huyu amefungua kesi katika kutuo cha Santa Monica police, anasema Stallone alitaka kum’baka mwaka 1990 katika ofisi yake, watu wa Rambo wamesema wanajua kuhusu kesi ya huyu dada na wanaamini anachotaka ni pesa tu, mpaka sasa Stallone amekanusha kutokea kwa tukio hilo.
Tokeo la picha la Sylvester Stallone
Fahamu kuwa muda wa kutoa taarifa ya makosa ya ubakaji baada ya kutokea mjini California ni ndani ya miaka 10 ya tukio, na sasa imepita miaka 27 kitu ambacho kitafanya ushahidi wa tukio hili kutopatikana kabisa.
Stallone amesema alitumia siku 3 kufanya filamu flani nchini Israel mwaka 1987, alikuwa Single muda wote na hakumuona mwanamke huyo.
Polisi wamethibitisha kuanza uchunguzi wa kesi hii

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top