Shehe Abubakary Zuberi Ally
.
Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir Bin Ally amesema Baraza kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA linaendelea kufuatilia kuandama kwa mwezi na kwamba litatoa taarifa kamili juu ya siku ya kufanyika kwa sikukuu ya Idd el-Fitr kama ni kesho au kesho kutwa.
Mufti, Aboubakar Zubeir Bin Ally ametoa kauli hiyo jana jioni kufuatia taarifa kupitia mitandao ya kijamii zilizozagaa na kusema kuwa sikukuu ya Idd el-Fitr itakuwa siku ya Jumatatu.
Mufti amesema hilo halijatangazwa na kufafanua kwamba Mufti ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza baada ya kushauriana na kamati ya mwezi.
.
source-est africa.tv

0 comments:
Post a Comment