Saturday, 24 June 2017

Mwanamitindo Jokate Mwegelo amefunguka na kuwataka wenye uwezo na wale wenye kipato.

Mwanamitindo Jokate Mwegelo amefunguka na kuwataka Watanzania wenye uwezo na wale wenye kipato kutojistarehesha wao wenyewe siku zote bali wawakumbuke na watoto  yatima na wale wote wanaoishi maisha magumu katika jamii. 


Jokate alisema hayo jana wakati akitoa msaada wa chakula na mavazi katika kituo cha yatima na wajane cha Ahbbabul Khairya kilichopo Mwananyamala Dar es Salaam ambapo aliweza kutoa mchele zaidi ya kilo 200, unga wa ugali kilo 250, mafuta ya kupikia, mbuzi wawili pamoja na nguo za watoto na wanawake.

    Msanii Jokate akiwa na baadhi ya wajane katika kituo cha Ahbbabul Khairya kilichopo Mwananyamala Dar es                   Salaam.

"Naguswa na changamoto mbalimbali ambazo Watanzania wenzangu wanakutana nazo kwa hiyo nakuja kutoa faraja lakini vilevile nakuja hapa kuwakilisha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu kule mimi ni kiongozi, kwangu mimi ni muhimu tunavyosherehekea sikukuu mara nyingi huwa tunajistarehesha wenyewe, kujinunulia nguo wenyewe lakini ukiangalia kwenye jamii kuna watu wengi wanapata changamoto mbalimbali ambao wanahitaji kuguswa na sisi" Alisema Jokate 
Kwa upande mwingine Mkuu wa Kituo cha Ahbbabul Khairya, Bwana Ahmed Shebe alishukuru na kumpongeza Jokate kwa kitendo chake hicho na kuwataka watu wengine wenye uwezo kuwakumbuka watu wenye mahitaji katika jamii ili kuwapa faraja na kuwatia moyo.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top