Sunday, 25 June 2017

Mchezaji wa liverpool watembelea yatima zanzibar


Familia ya beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England jana Jumamosi imetembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS kilichopo Mombasa, Unguja.

Sakho amefuatana na mke wake Madna na watoto wake wawili wa kike.

Sakho akiwa Zanzibar alizindua mashindano ya Coco Sports Ndondo Cup mchezo ambao Taifa ya Jang’ombe walifungwa 2-1 na Mlandege SC.

Sakho yupo  visiwani Zanzibar tangu  Juni 17, kwa ziara ya kiutalii. Awali ziara hiyo, alianzia Tanzania Bara kisha kurejea Ufaransa na baadaye kurudi Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top