Sunday, 25 June 2017
Johhny Depp aomba radhi kwa kutaka kumuua Rais Trump
Mwigizaji maarufu Hollywood Johnny Depp ameomba radhi baada ya kutoa utani mbaya juu ya kutaka kumuuwa rais Donald Trump.
Kwenye interview kwenye Glastonbury 2017 Johnny Depp alitania kwa kusema , “Tunaweza kumleta Trump hapa, nadhani anahitaji msaada, ni swali tu, sio kwamba nataka kutukana mtu ila lini ni mara ya mwisho mwigizaji kumuua rais? “
Kauli hii ilichukiza wafanyakazi wa Rais ndani ya White House na kutoa malalamiko yao juu ya usalama wa Donald Trump.
Johnny Depp ameomba radhi baada ya msemaji wa White House kulalamikia HollyWood kuhusu mwigizaji wao. Johnny anasema “Naomba radhi kwa utani mbaya juu ya rais, sikuwa na mpango wa kufanya nilichosema, nilitaka kuchekesha sio kudhuru mtu“.
Johnny Depp ni miongoni mwa waigizaji wa kubwa Hoolywood, anayepewa filamu kubwa na kulipwa zaidi.

0 comments:
Post a Comment