Mkimbizi mmoja kutoka Burundi, Bella Nshimirimana amepata tuzo ya kuwa mwanamke mkimbizi bora nchini Uganda mwaka huu wa 2017, kutokana na mchango wake katika masuala mbalimbali yenye tija kwake mwenyewe na kwa jumuiya nzima ya wakimbizi. Miongoni mwa mambo hayo ni kuwasaidia wakimbizi wenzake kufanya shughuli halali za kujiingizia kipato, na kuwasaidia wagonjwa wasioelewa lugha ya nchi mwenyeji kuzungumza na wauguzi ili wapate nmatibabu yanayofaa. Mwandishi wetu Lubega Emmanuel kutoka Kampala atatuletea zaidi katika matangazo yetu ya mchana huu.

0 comments:
Post a Comment