Friday, 23 June 2017

Jokate Mwegelo, ameweka wazi kuwa anatamani kuwa na watoto mapacha

Mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo, ameweka wazi kuwa anatamani kuwa  na watoto mapacha katika maisha yake.
Jokate ameliambia Gazeti la Mtanzania kuwa mwanamume atakayekuwa mume wake atamuweka wazi hivi karibuni lakini anapenda wawe na watoto mapacha atakaowalelea kijijini.

“Kuna umri ukifika unajikuta unatamani kupata mtoto, napenda nipate watoto mapacha na wote niwalee maisha ya kijijini na mjini ili wajue maisha ya pande zote. Napenda niwalee watoto hao maisha ya kijijini ili wajifunze kilimo, kula chakula vya asili na wajifunze tabia nzuri na za kupendeza jamii,” alieleza Jokate.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top