Saturday, 24 June 2017

Kenya inasema washambuliaji wamewapiga risasi na kuwauwa watu watatu.

Polisi nchini Kenya inasema washambuliaji wamewapiga risasi na kuwauwa watu watatu wakati wa uvamizi wa benki moja ya kibiashara kaskazini mashariki mwa nchi hiyo hivi leo.

Waliouawa ni raia wawili na afisa mmoja wa polisi katika mashambulizi hayo kwenye Kaunti ya Mandera, kwa mujibu wa kamanda wa polisi, Charles Chacha.
"Kulikuwa na majambazi watano wenye silaha. Walipofika kwenye benki, walimpiga risasi afisa wa polisi aliyekuwapo mlangoni, na polisi walifanikiwa kumpiga risasi mmoja wa wahalifu hao, lakini...walikimbia," Chacha aliliambia shirika la habari la Reuters.
Elwak, mahala hasa ambapo mashambulizi hayo yametokea, pako karibu na mpaka wa Somalia.
Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu linasema pia kuwa bomu lililotegwa barabarani limelipuka kwenye mji huo huo wa Mandera, ingawa hakuna taarifa za waliouawa ama kujeruhiwa kwenye mlipuko huo.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top