Sasa msanii Nikki wa Pili ametoa maoni yake kuhusu kauli hiyo ya hitmaer huyo wa Hela, kwa kusema si kweli kwamba muziki amepata kilema kwani muziki unakuzwa na vipaji na sio tuzo wala albamu.
“Tuzo au albamu ni vitu vya kusogeza tu lakini pia albamu hazijatoka kutokana na matatizo ya kisoko lakini sio kama muziki wetu umepata kilema. Mimi naona muziki ndani ya talent za wasanii wenyewe as long as una kipaji kikali utakuwa na muziki mkali. Unaweza kuwa na tuzo na albamu lakini kama huna talent huwezi kuwa na muziki.
.
“Hivyo vitu sivikatai vinasaidia muziki lakini muziki unaanza vipi? Je kuna watu wenye talent, maprodyuza wakali, kuna watu wenye uwezo wa kuimba na ku-deliver muziki mzuri, muziki utatusua,” ameongeza.

0 comments:
Post a Comment