Thursday, 6 July 2017

Watu wa wili wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa, Baada ya kutokea ajali ya Basi la UPENDO

Watu wawili wamefariki dunia na wengine wanane wamejeruhiwa baada ta basi waliokuwa wamepanda la kampuni ya Upendo kuacha njia na kupinduka Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya, Reuben Mfune amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo cha ajali hiyo kimetokana na mwendo kasi wa dereva ambapo basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam.
Pamoja na hayo, Mfune amesema majeruhi wa watano ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Misheni ya Chimala ya Wilaya ya Mbarali
na wengine watatu wamepelekwa Hospitali ya Rujewa kwa matibabu.
.
.
.
source-eatv

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top