Hit maker wangoma ya Aje amesema hayo baada ya kuulizwa kwamba kwa sasa
hawaonekani kuwa karibu na Baraka kama zamani huku tetesi zikidai kwamba
ukaribu wao umevunjika baada ya Alikiba kuwa karibu na Ommy Dimpoz.
Alikiba alisema “Mimi nadhani ni utoto tu, nadhani ni umri tu lakini Baraka yupo vizuri,
ni mtu anayesikiliza na ana rekebishika. Muda mwingine labda umri ndio
unampeleka lakini muda mwingine mtoto akifanya jambo unamwambia,”
Alikiba alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM. “Ni mdogo wetu
tutamwelimisha na sidhani kama anamchukia Ommy Dimpoz labda ni maneno tu
ya mtaani,”
.
Na Kwa upande wa Ommy Dimpoz ambaye alitambulisha wimbo wake mpya Cheche,
amedai yeye hajawahi kugombana na Baraka na wala hana tatizo na mtu
yeyote.

Braka bado anawenge la ustar ila atakuwabado mdtoto kweli uyo
ReplyDelete