Tuesday, 4 July 2017

Hatua za kufanya ili kijana ufanikiwe katika maisha yako


1:KIJANA JITAMBUE
Pana kila sababu ya kijana kujitambua maana kijana anapojitambua anakuwa na uwezo mpana wa kuchanganua mambo kiyakinifu, anakuwa na uwezo wa kuona mbali ki-fikra..
Kijana ambae hajitambui hata ukimpa mtaji wa mabilioni ya pesa hawezi kufanikiwa.
Mungu amekujalia akili na nguvu je kwanini usijitambue..jiulize vilema wangapi wanafanya kazi na kufanikiwa wewe uliebarikiwa kila kitu na Mungu wako kwanini usifanye na kufanikiwa? Yote haya yanatokana na kutojitambua kama kijana ...utakuja kujitambua muda ukiwa umeshakuacha ndio utajipa moyo muda unao lakini akili na mwili vitakua vimechoka vimekata tamaa vyote kwa pamoja.

Paul Gascoine "Gazza" mchezaji mpira  maarufu wa Uingereza na vilabu 9 tofauti..kipindi akiwa kijana alijaliwa kipaji ndani ya miguu yake na aliweza kukitumia vizuri kwa kuwapa mashabiki wake wanachohitaji na yeye aliingiza fedha kupitia miguu yake uwanjani lakini tatizo hakujitambua Gazza, hakutambua kuwa mpira ni mchezo wa muda mfupi hakutambua kuwa kuna maisha baada ya mpira akajikuta anatumia pesa zake kwenye ulevi  wa pombe uliopindukia..alicheza mpira kwa mafanikio lakini hakuyaona mafanikio yake Gazza alikosa kitu kichwani mwake na kitu alichokosa ilikua KUJITAMBUA yeye kama yeye alijikuta akizitambua pombe zaidi kuliko yeye mwenyewe. Endapo Gazza angejitambua angekuwepo mbali kimaisha kama Antonio Conte Mourinho hata Guardiola na ana umri wa miaka 49 kwa sasa lakini maisha yake ni kama ameishi karne moja.

Vijana tuna mifano mingi ya kuangalia na kujifunza kwa vijana wenzetu ambao hawakujitambua na sasa wanaishi maisha yaliowachagua na sio waliyoyachagua mfano kama Chid Benz na  Daz Baba. Sidhani kama kuna mtu anatamani maisha kama hayo

Mifano hiyo hapo juu ni hasara za kutojitambua kama vijana lakini endapo utajitambua ukajua umekuja duniani kufanya nini na unatakiwa kuwa wapi Mungu yu pamoja nawe hakika utafanikiwa.

Kumbuka ukishindwa kujitambua na mafanikio pia yanashindwa kukutambua



2:KIJANA ISHI NDOTO ZAKO
Kijana mmoja alikua na ndoto siku moja awe mwandishi wa filamu na muigizaji mkubwa nchini Marekani..
Alijaribu kuandika baadhi ya filamu nyingi na kuzipeleka kwa waongozaji filamu wakubwa kipindi hicho lakini kila alikua akipeleka inakataliwa.
Watu wengi walimuona anapoteza muda na fedha nyingi za kufatilia mambo ambayo anakataliwa yeye hakukata tamaa ilikua ni ndoto yake lazima aishi ndani yake...
Ilifika kipindi hela zilimuishia aliamua kumuuza mbwa wake kwa thamani ya dola za kimarekani $50 aliumia sana kumuuza mbwa huyo ambae alikua kama rafiki kwake ila alikua tayari kupoteza kila kitu ili aishi ndani ya ndoto zake.

Baada ya kumuuza mbwa yule na kwa hela ile alifanikiwa kupeleka filamu yake na mwisho wa siku ilikubaliwa lakini alikataliwa asiigize yeye aliambiwa hana muonekano mzuri wa kuigiza..alivoambiwa vile alichukua filamu yake na kuondoka alikataa kuwauzia sababu lengo lake ni kuigiza pamoja na yeye awe muigizaji bora duniani hakutaka kuuza tu ili apate pesa maana kama ni pesa hakushindwa kuzitafuta au kwenda kuajiriwa mahali na alkua ana shahada yake..lengo lilikua ndoto zake zitimie... Muongozaji mmoja alimuita kijana yule na kumuambia kama yupo tayari kuigiza bas asiuze ule muongozo wa filamu bali awape bure na yeye ataigiza hela yake atapewa baada ya mauzo ya filamu yake..kijana alikubaliana na hilo kwa mikono miwili alikubali hatimaye akacheza filamu ile na ikawa filamu bora kwa kipindi hicho aliingiza fedha nyingi sana alirudi na kumnunua mbwa wake yule mara mbili ya hela aliyomuuzia $100...kijana huyo ni mtu mkubwa na anaheshimika mpaka sasa ndani na nje ya marekani kutokana na kazi zake za filamu hapo namzungumzia SYLVESTER HALLONE  jina maarufu kama RAMBO..



Tujifunze kuishi ndani ndoto zetu kama RAMBO  vijana mara nyingi tunazikimbia ndoto zetu kwa sababu unahofia kupoteza muda..unahofia kuchekwa na ndugu au marafiki hapo ndo tunajikuta tunaishi ndani ya ndoto za watu wengine..ukiishi ndani ya ndoto ya mtu mwingine hutapata furaha ya maisha kamwe sababu wakati mwingine ndoto za mtu huyo ni mbaya na za kutisha....



Ndoto za mtu zinaumiza sababu utafanya kitu ambacho maishani kwako hakikupi raha hata kidogo..

Huwezi kutamani kuwa msanii wa muziki mkubwa halafu uone raha ya kuwa mtangazaji.. Watu wengi hawana furaha maofisini sababu kazi wanazozifanya sio moja ya ndoto zao ila anafanya sababu anaitaka pesa tu... Pesa tamu ni ile unayofanya kazi unayoipenda na siku zote kazi unayoipenda unaifanya kwa makini zaidi..


Sikushauri uache unachofanya kwasasa hapana sababu kuacha ni maamuzi yako binafsi ila ukiamua kuacha mwenyewe na kufanya unachopenda pia ni vizuri zaidi


3:KIJANA EPUKA MAISHA YA KUIGIZA

Maisha ya kuigiza kwa vijana wengi wa kitanzania kwasasa ni kawaida sana na wengi ndicho kinachowapotezea dira ya maisha..
Kuna mtu anawaza atakula nini sababu hakuna hela lakini akiona nguo mpya kavaa msanii mkubwa mfano @diamondplatnumz  yupo tayari asile lakini avae nguo zile...Maisha haya ni ya kuigiza bila sababu..

Ukifikiria kipindi @diamondplatnumz hajafanikiwa kuwa msanii mkubwa alikua havai nguo za gharama alikua anakusanya hela kwa ajili ya kurekodi nyimbo zake na alifanikiwa na sasa anaweza kuvaa nguo za gharama anavyotaka..

Kila mtu anayatamani maisha mazuri na matamu lakini lakini ni lazima upambane ili upate unavotamani
Vijana wengi wanapoteza muda na pesa nyingi sana kwenye maisha ya kuigiza avae aonekane kama nani aongee kama nan wengine hufika mbali na kuacha vipaji au vipawa walivyojaliwa na Mungu na kufanya vingine ili waonekane kama mtu fulani  ukweli ni kwamba utafeli kijana mwenzangu maisha hayaigizwi bali yanafanywa kweli....

Muda na akili vijana wanayotumia kupata hela na kununua suruali tishet na kofia kama ya Diamond au simu kama ya @juma_jux  akili hizo na muda huo wangewekeza katika kutafuta pesa kwa ajili ya maisha ya baadae huenda wangeishi maisha makubwa kuliko hao
Aliwahi kusema mtu mmoja maarufu kwasasa ni matehemu STEVE JOBS mmiliki wa kampuni ya Apple alisema hivi "Your time is limited, so dont waste it living someone else's life." ( Muda wako ni mdogo/hautoshi hivyo usiupoteze kwa kuishi maisha ya mtu mwingine)

Usiishi maisha ya kuigiza kijana mwenzangu muda unaouona mwingi ni mchache sana  ishi maisha yako kwa sasa ili baadae watokee watakao kuigiza wewe


Sio vibaya kufata njia za mafanikio aliyopata mtu ila ni vibaya kuishi kwa kumuiga yeye


4: KIJANA FIKIRIA MAWAZO CHANYA KILA SIKU
Watu wengi hufikiri muda walionao ni mwingi sana katika maisha hivyo hujikuta hutumia muda huo katika mambo hasi bila kujua kuwa muda walionao ni mchache sana tena huwa mchache zaidi kwasababu hujui siku wala saa ya kwako kuishi duniani. Unapoutumia muda uliopewa bure vibaya kwa sasa jua kuwa utautafuta muda huu baadae kwa gharama yoyote ila utakuwa ushachelewa  na malipo ya muda huu baadae ni kuishi maisha ya kujuta siku zote.. Mfano  Vijana hutumia muda mwingi kufanya starehe zinazomaliza hela badala kufikiri  jinsi ya kuongeza hela. Kumaliza hela tena kwenye starehe ni rahisi sana kuliko kuongeza hela.. Wengi huja kutambua hili mwishoni wakati wa majuto ...starehe zote za anasa ni hasi haziwezi kubadilika kuwa chanya hata siku moja......mawazo hasi ni adhabu ya mwili na ubongo. (Tafakari kuhusu hilo)

  Unapofikiria kuwa na gari zuri nyumba zuri mke mzuri hayo halafu hatendei kazi unavyofikiria hapo hujakamilisha fikra chanya

Kuwa na mawazo chanya, fikiria chanya, fanya chanya,nawe utakua chanya kwenye maisha yako.
Mawazo chanya yanakupa furaha maishani kwako ..mtu mwenye mawazo chanya huwa na uwezo wa kukamilisha ¾ ya malengo yake yote aliyopanga sababu mtu mwenye mawazo chanya huona fursa nyingi katika maisha yake

Leo tuishie hapa kesho tutamalizia njia nyingine nne ... Ungana nasi kila siku
Asante!



1 comment:

  1. Kujielewa ni borazaidi kwa kijanasafi sana Broo Jayspeed mnafanya vitu vikubwa sana hamjuituu

    ReplyDelete

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top