Thursday, 6 July 2017

KIDUDU MTU AONEKANA MOSHI

Mdudu ambae amekua akiongelewa sana mitandaoni na baadhi ya video zake kutumwa, mdudu huyu ambae alikua akionekana kwenye mbogamboga baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa kama geita na sehemu nyingine leo hii mkazi mmoja wa mjini moshi baada ya kununua mboga zake za majani wakati anazichambua mkazi huyo alimuona mdudu huyo. Mkazi huyo alitoa taarifa kwa watu na taarifa hizo zilitufikia  Lambegu blogspot na bila kupoteza muda tulifika eneo hilo na kushuhudia mdudu mtu huyo ambae anadaiwa kuwa hatari endapo mboga hizo watu watakula  inaweza kuwasababishia kupoteza maisha kwa muda mfupi tu.. Lambegu blogspot bado tunajitahidi kuwatafuta wataalamu zaidi watuambie kuhusiana na wadudu hawa kuingia ndani ya mji wa Moshi...

Onyo: usile mboga za majani bila kuzichambua vizuri na kuziosha kwa umakini kwani unaweza kukutana na kiumbe hiki  hatari .

2 comments:

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top