Jana tuliishia njia Nne za kijana kufata na kufanikiwa kwenye maisha yake leo tutae delea njia nyingine Tatu na za mwisho karibu tuwe pamoja katika sehemu hizi..
5: KIJANA TAMBUA VITU VIPYA KILA SIKU
Njia ya kutambua vitu vipya kila siku ni kusoma vitabu sana au kujifunza kila mara chochote unachoona ni kigeni kwako na hapa watu wengi wanaposhindwa ukimwambia mtu soma vitabu anasema hana muda wa kusoma au anaona uvivu kusoma kama huna muda au sio mpenz wa vitabu jaribu kusikiliza sauti zilizorekodiwa (audio) za watu waliofanikiwa hapo utajufunza mengi mapya kuanzia mbinu na hatua za kufanikiwa ..
Tambua kuwa hata kama unafanya kazi yako usipokuwa unajifunza mambo mapya kila siku kazi yako itakuwa haiendelei maana ubongo wako utakuwa unafanya kazi hiyo kwa mazoea hutakuwa na mbinu mpya za kuongeza kipato chako, kila siku utakuwa unalalamikia kuwa biashara ngumu huku upande wengine wanaofanya biashara kama yako wanazidi kufanikiwa.. Jifunze mambo mapya na jitahidi kuyatimiza. Kila siku watu watakuona mpya hata ukiwa unaongea watu hutamani kukusikiliza maana unaongea mambo mageni masikioni mwao..
Kuwa mdadisi zaidi katika mambo yenye faida kama ni mfanya biashara idadisi kila siku na jifunze zaidi biashara yako vivo hivyo kwa mwalimu, daktari na hata mwanasheria jifunzeni zaidi mambo mapya ..kusoma darasani kuna mwisho lakini tambua kujifunza hakuna mwisho ukiona umefikia mwisho wa kujifunza tambua umeanza kuzeeka hata kama ni kijana utakuwa kijana mwili lakini akili itakuwa imezeeka maana hakuna kipya kinachoingia katika ubongo wako aliwahi kusema mgunduzi wa magari maarufu Henry ford
"Anyone who stops learning is old, whether at twenty or eighty. Anyone who keeps learning stays young" (yeyote ambaye ameacha kujifunza ni mzee haijalishi ana miaka ishirini au themanini. Na yeyote ambae anajifunza bado hubaki kijana.) Mungu kakujalia muda na akili yenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya mambo milioni zitumie vizur akili zako katika kujufunza mambo mapya
Kutambua vitu vipya kila siku kutakufanya utambue mbinu nyingi za kupambana na maisha...poteza robo tatu (¾) ya siku yako katika kujifunza mambo mapya na kuanza kuyafanyia kazi. robo ¼ ya siku iliyobaki igawanye tena nusu ya robo hiyo itumie kuongea na familia yako kila siku na iliyobaki itumie kwenye mambo yako unayojua mwenyewe..
6: KUBALI KUKOSOLEWA NA SAHIHISHA ULIPOKOSEA
Ili kujua ulipokosea kubali kukosolewa siku zote. Unapokosolewa lazima usahihishe makosa yako hautakuwa tayari kuonekana mtu wa makosa kila mara.
Kama ilivyo kwenye mpira wa miguu timu inapofungwa huwa imefanya makosa na goli kutokea wanapotoka uwanjani wakiwa wamepoteza jambo lile huwatafuna mioyo yao hvyo wanaenda kutafuta walipokosea na wana sahihisaha wanaporudi tena uwanjani hiubuka na ushindi na maisha ndivo yalivyo siku zote unapokosea kwenye maisha yanakupiga lakini unapolijua kosa lako na kurekebisha unafanikiwa.....
Hebu fikiria Mafanikio makubwa anayoyapata Jack Ma ndani ya kampuni yake ya Alibaba mpaka sasa yote hayo ni kufanyia kazi makosa yake aliyokosolewa kwenye kazi 30 alizoomba na kukataliwa kote..alijiuliza kwanini na ni wapi hasa anakosea mpaka mashirika 30 yanamkataa kwenye kazi hizo? alijua alipokosea na akafanyia kazi makosa yake sasa hivi ni moja ya matajiri wakubwa duniani na tajiri zaidi ndani ya China....
Kukubali kuwa umekosa haimaanishi wewe ni mjinga au huna akili la hasha! Inamaanisha wewe ni shujaa... Shujaa ambae umekiri kweli umefanya kosa hilo na sasa umejifunza kupitia kosa hilo..
Jifunze kupitia makosa yako rekebisha ikiwezekana uanaposhindwa omba ushauri kwa watu wa karibu ...kumbuka kukumbatia kosa lako moyoni ni ugonjwa, ugonjwa ambao unakuangamiza taratibu na mwishoni kufa kwa aibu
7: UKITOA TOA BILA KUKUMBUKA
Neno KUTOA lina herufi tano ambazo ni chache sana kuliko milioni, utajiri, na kufanikiwa lakini neno hilo ndilo linatengenezea watu maneno yote hayo yenye faida... Jambo la kutoa ni moyo wala sio mali ulizo nazo au mafanikio yako uliyonayo......, unaweza ukawa huna mali lakini maneno yako kuyatoa kwa mtu yakawa na thamani zaidi ya mali..
Kutoa ni moyo naposema ni moyo namaanisha lazima uwe na moyo wa kuhifadhi ulichotoa yaani ulichotoa kibaki moyoni mwako usikumbuke ulichotoa..unapokumbusha ulichotoa au kusema kwa watu kuwa umemsaidia mtu fulani jua kuwa sio msaada bali ni deni unalitangaza na unataka fadhila zako ulipwe.. Toa msaada bila kukumbuka na uliemsaidia akifanikiwa hatasita kuelezea msaada wako kwa watu... Benjamini Graham hakutangaza kumsaidia Warren Buffet lakini Buffet alipofanikiwa alitangaza kuwa kufanikiwa kwake mbali na jitihada zake lakini kuna mtu alieitwa Benjamini aliechangia yeye kufanikiwa zaidi...kumtangaza aliekusaidia sio mbaya ila kumtangaza unaemsaidia ndio mbaya hata kiimani dini zote zinakataza hilo.. Wewe amini kuwa Unapotoa msaada mfano kusaidia watu wa tano wafanikiwe jua kuwa umesaidia familia tano za kitanzania kufanikiwa na ndani ya familia hizo zitasaidia wengine wewe baki kuamini hivo lakini usiangalie nini kinaendelea.. Ishi kwa kuwa msaada wa jamii sio kwa ulicho nacho bali kwa ulichojaliwa na Mwenyezi Mungu nae Mungu atazidi kukujalia kila siku .
0 comments:
Post a Comment