Friday, 14 July 2017

Mtandao wa Instagram umesababisha wasanii wengi kuchukuliwa poa

Young Killer Msodoki amedai mtandao wa kijamii wa Instagram umesababisha wasanii wengi kuchukuliwa poa na mashabiki hasa wa hip hop kwa kuwa wanachokipenda zaidi ni umbea kuliko kufuatilia kazi za msanii mwenyewe anazozifanya katika muziki wake.
Rapa Young Killer Msodoki.
Young Killer amebainisha hayo baada ya kuwepo dimbwi kubwa la mashabiki kufuatilia na kuchimbua maisha binafsi ya wasanii na kuwaanika katika mitandao mbalimbali ya kijamii jambo ambalo limepelekea watu kupenda 'udaku' zaidi kuliko hata kujua ni kazi gani mpya ya msanii ameitoa au anaifanya kwa kipindi hiki.
"Now days watu wamekuwa wanapenda vitu vya hovyo sana yaani vile vitu 'real' ambavyo vinafanya sisi tuwe katika nafasi ambayo tulikuwepo vinakuwa vinapotezwa na vitu vya 'kipumbavu' sana", amesema Youngkiller.
Pamoja na hayo, Young Killer ameendelea kwa kusema "mitandao imekuwa mingi, maisha yetu yote sasa hivi watu wanatuchukulia poa tu, so hiyo nadhani inachangia kushusha hata 'mode' ya kufanya kazi nzuri". Alisema Youngkiller

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top