Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro amesema kuwa watumishi hao 450 ni kati ya watumishi 1500 ambao walikata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ya serikali ya kutaka watumishi wenye vyeti feki kuacha kazi na kusitishiwa mishahara yao.
"Kati ya hao wengine walikuwa ni wale ambo wameolewa na kupata majina ya waume zao kwa hiyo baada ya kuolewa majina ya wanaume zao yakawa yanatofautiana na majina yao yaliyopo kwenye vyeti, kwa hiyo wakati ule vilikuwa vinaonekana vile vyeti kama si vyao na kwa bahati mbaya Watanzania wanapoolewa wanachukua majina mawili ya wanaume zao badala ya kuchukua jina moja. Lakini pia kulikuwa na wengine majina yao ya kidato cha nne na kidato cha sita yalikuwa tofauti" alisema Ndumbaro
.
.
.
.
source>>eatv
.

0 comments:
Post a Comment