Wakati wa mechi ya Azam 1-0 Kagera Sugara, golikipa Juma Kaseja alionekana akiwa amevaa gloves zenye jina lake (Kaseja) zilizotengenezwa na kampuni ya Nike ambayo ni maarufu duniani kwa utengenezaji wa vifaa vya michezo.
ShaffiDauda.co.tz ikataka kujua kama Kaseja anamkataba wowote na Nike kwa ajili ya kuvaa bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo.
“Hakuna mkataba wowote, hizi gloves nimenunua mwenyewe nikaenda sehemu ambapo huwa wanaprint majina nikaandika jina langu lakini sio kwamba natengenezewa special na Nike”-Kaseja.
Ni jambo la kawaida kwa wachezaji wa Ulaya na sehemu nyingine zilizoendelea duniani kuona mchezaji amevaa viatu, gloves na vitu vingine vikiwa vimeandikwa jina lake na kampuni husika ya utengenezaji wa vifaa hivyo.

0 comments:
Post a Comment