Friday, 15 September 2017

“Mimo ndio nahusika na wachezaji, Tevez amekuwa mnene " Wu Jingui

Carlos Tevez alinunuliwa kutoka Boca Junior kwa kiasi cha £78.2m kwenda Shanghai Shenhua usajili ambao karibia kila mtu aliamini sasa ligi kuu ya China inakwenda kushuhudia idadi kubwa ya mabao.
Lakini jambo la ajabu kwa mwanasoka huyu anayelipwa zaidi duniani ni kwamba amefunga mabao 2 tu tangu asajiliwe na klabu hiyo December 29 mwaka jana huku hadi sasa akiwa amevuna kiasi cha £23,680,000 tangu ajiunge na Shenghua.

Badala ya Tevez kujituma na kuonesha thamani yake uwanjani lakini sasa mchezaji huyo ameamua kutumia pesa hizo katika masuala mengine nje ya uwanja ambayo yamempelekea kuanza kuwa mnene.

Kocha mpya wa Shanghai Shenhua Wu Jingui ameona inatosha na sasa hajali kuhusu kiasi ambacho Carlos Tevez amesajiliwa ambapo kuanzia sasa kocha huyo ameamua kumuweka benchi Tevez hadi atakapokuwa fiti.

“Mimo ndio nahusika na wachezaji, Tevez amekuwa mnene na kama hauko fiti kwa 100% hiyo haina maana yoyote wewe kuwa uwanjani inabidi ukae nje” alisema Wu.

Wu Jingui amechukua mikoba ya Gus Poyet aliyebwaga manyanga, na Wu anaonekana hajali kuhusu ukubwa wa Carlos Tevez ambaye kwa wiki anapokea kiasi cha £640,000.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top