Moja ya wa memba kutoka kundi la muziki wa Hip Hop Bongo, Sisi Sio Kundi (SSK), P The Mc amesema kuwa alipata ruhusa zote kutoka kwa prodyuza mkongwe P-Funk Majani kabla ya kurekodi ngoma ya ‘Mademu Wangu’.
Akiongea na Bongo5, P The MC amesema yeye ni shabiki mkubwa wa marehemu Ngwear na amefanya ngoma hiyo kama kumuenzi na pia amepokea bless zote kutoka kwa P- Funk Majani kabla na baada ya kuachia wimbo huyo.
“Mimi nilikuwa natafuta connection ya Ngwear, kwa kuwa siku-exit kwa nafasi kubwa sana kipindi chake ndiyo maana sikupata hiyo fursa, ila kwa sababu wazo nilikuwa nalo nikaona nitumia hiyo fursa kama yeye hayupo sasa hivi , so nilichofanya ni kuchukua wimbo kutoa kwenye albamu yake ya ‘A.K.A Mimi ‘ unaitwa ‘Mademu Wangu’ nikaufanyia remix ambapo nimetumia beat hiyo hiyo na Ngwear akibaki kwenye kiitikio hivyo hivyo. The idea ni ileile isipokuwa Ngwear aliwaongelea mabinti kutokana na makabila yao mimi ni meongelea mabinti kutokana na tabia zao,” amesema msanii huyo.
Pia akaongeza “Ruhusa ya kurekodi wimbo huo nilipata kutoka kwa Majani, C.E.O mwenyewe ambaye tulianza kumshirikisha kwenye suala hili kabla ya kurekodi na akasema, rekodini wimbo harafu mnitumie nisikilize kama kutakuwa na chochote cha kuongeza ama kupunguza nitawaambia na kama utakuwa sawa nitawaruhusu, so tukamtumia P-Funk akausikiliza na akasema hauna tofauti yoyote wimbo mzuri na nimeupenda mnaweza mkau-push vyovyote mnavyotaka lakini tu kama utaingiza pesa basi hiyo pesa iyende moja kwa moja familia ya Ngwear.”
Akasisitiza “P-Funk akaongea na Mkito.com ambayo ndiyo platform ya kuuza wimbo huo na Mkito.com wakafungua akaunti kwa ajili ya Ngwear na sio yangu wala ya P na hiyo akaunti inaitwa Mangwear.”
0 comments:
Post a Comment