Akizungumza katika maadhimisho hayo Mstahiki meya wa manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta ameeleza kuwa licha ya kuwapatia vitambulisho hivyo, amesema imewekwa mikakati maalumu ya kutambua changamoto nyingine za wazee ili waweze kuwawezesha wazee hao, ambapo pia amewashuri wajiunge katika vikundi ili iwe rahisi kuwafikia
Akisoma risala hiyo kwaniaba ya Wazee kata za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Nassoro Juma Mataula wameishukuru serikali kwa hatua hiyo ya kuwapatia kadi za matibabu kwakuwa wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wengine hadi kupoteza maisha.
Aidha wazee hao wameiomba Serikali kuwapa kibali kitakachowawezesha kusafiri bure au kufutiwa nauli za mabasi ya mwendo kasi, Mabasi yaendayo mikokani sambamba kuongezewa pensheni.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Festo John Dugange amesema zoezi hilo ni endelevu ambapo amewaomba wazee wajitokeze kwa wingi katika Ofisi ya Halmashauri au ofisi za kata zao ili kutambuliwa na kupewa vitambulisho vya matibabu bila malipo.
0 comments:
Post a Comment