Bodo Mende na Karl Kreile wakila kiapo kanisani.
Tukio hilo la kufunga ndoa kwa mashoga hao wawili waliotambulika kwa majina ya Bodo Mende (60) na Karl Kreile (59), limekuja miezi michache baada ya bunge nchini humo kupiga kura ya kuruhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Awali wapenzi wa jinsia moja nchini Ujerumani walikuwa wakisajili uhusiano wao tangu mwaka 2001, hadi mwezi Juni mwaka huu wakati bunge lilipopiga kura ya kuwepo usawa wa ndoa jinsia moja.
Mamia ya wanawake (Wasagaji) wakishangilia mapema mwezi Juni mwaka huu baada ya bunge la Ujerumani (Bundestag) kupitisha sheria ya ndoa ya wapenzi jinsia moja.
Tukio hilo la kufunga ndoa kwa mashoga hao wawili waliotambulika kwa majina ya Bodo Mende (60) na Karl Kreile (59), limekuja miezi michache baada ya bunge nchini humo kupiga kura ya kuruhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Awali wapenzi wa jinsia moja nchini Ujerumani walikuwa wakisajili uhusiano wao tangu mwaka 2001, hadi mwezi Juni mwaka huu wakati bunge lilipopiga kura ya kuwepo usawa wa ndoa jinsia moja.
Hata hivyo hatua hiyo ya Bunge kuruhusu ndoa ya jinsia moja haukuungwa mkono na Kansela wa Ujerumani, Bi Angela Merkel pamoja na baadhi ya wabunge wa chama chake cha CDU huku vyamala pinzani vikipiga kura kwa wingi kuruhusu ndoa ya jinsia moja.
Sherehe hizo za ndoa ya jinsia moja hazikuishia kwa wananchi tu kwani hata Msemaji na Mwenyekiti wa Chama cha haki za wanawake nchini humo Bi. Anja Kofbinger amepongeza wanandoa wengine wa kwanza wanawake (Wasagaji) huku akisema kuwa safari iliyokuwa ikisubiriwa tayari imeanza.
Kwa mujibu wa takimu zilizotolewa na Yahoo mpaka sasa hivi nchini Ujerumani kuna watu 94,000 ambao wamejisajili kuwa wanahusika na mapenzi ya jinsia moja na wote wanatarajiwa kufunga ndoa.
Ndoa za jinsia moja zitawaruhusu wapenzi hao kupata haki sawa ikiwemo ya kuasili watoto kama ndoa za kawaida zinavyofanya.
Ujerumani inakuwa nchi ya 15 barani Ulaya kupitisha sheria ya ndoa ya wapenzi wa jinsia moja.
0 comments:
Post a Comment