Tuesday, 14 November 2017

Haya ndio majibu ya Mrisho mpoto baada ya Post ya Afandesele.

Tokeo la picha la mrisho mpoto
Baada ya muigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael Lulu kuhukumiwa kifungo cha miaka 2 jela kutokana na kukutwa na hatia ya kusababisha bila kukusudia kifo cha Steven Kanumba, mwaka 2012. Afande amemrushia lawama marehemu Kanumba na kudai kuwa alistahili alichokipata kutokana na kuwa na uhusiano na mtoto mdogo.
>>Hichi ndicho alicho andika Mrisho Mpoto Katika mtandao wake wa Instagram kumjibu msanii Afande Sele Theking aka yangu Afande Sele.. Mfalme wa maandishi…!! @afandeseleking Wewe ni Kaka yangu na ni mwandishi ambae sijawahi kuacha kuheshimu maandishi yako …Leo nna mambo kadhaa kidogo kwako Kaka yangu…. Nimesoma maandishi kwenye ukurasa wako zaidi ya mara 30 Huku nikiyarudia rudia mara Kadhaa…ningependa kujua vitu Vichache kabla ya hoja yangu ya msingi kuiweka mezani…ile Barua ulimwandikia Marehemu Kanumba ulitaka imfikie? Au ulitaka wanaokwenda nyuma yake wamfikishie? ulitaka waliopo wajifunze kupitia walaka wako? Mbona nimepata kusikia Marehemu huwa halaumiwi kwakua hana uwezo wa kijitetea? Umesema ulikuwepo Sinza wakati wa msiba na hukutaka kusogea wala kuzika kwakua unasema wewe siyo mnafiki kama watanzania waliokwenda kuzika… ikiwa watu wote wangekataa ile Maiti ingekuaje? Nini Hasa lengo la Movies za Kibonge kuziita Maigizo yanayowekwa Kwenye Kanda? una ugomvi na Bongo Movies au uliandika ukiwa kwenye Jazbda kidogo….!! Mimi ndugu Mrisho Mpoto

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top