Saturday, 18 November 2017
Mshindi wa Bajaj ya promosheni ya Shinda na SportPesa kutoka Bukoba akabidhiwa zawadi yake
Wilson Wincheslaus Ngemela mfanyabiashara na mkazi wa Nyamkazi Bukoba (21), Mshindi wa droo ya 14 kwenye promosheni iliyofanyika tarehe 8 Novemba mwaka huu amebadilisha maisha yake kwa kueleza jinsi alivyonyakua zawadi hiyo ya Bajaj.
Kadri siku zinavyoendelea, Promosheni ya Shinda na SportPesa imekuwa ikipamba moto kwa kubadilisha maisha ya Watanzania. Mpaka sasa washindi 23 wameshapatikana na baadhi wameshakabidhiwa bajaji zao aina ya TVS King Deluxe. Watu wa rika zote wamejitokeza kushiriki katika droo hiyo kwa kuweka ubashiri na SportPesa kisha kutuma neno Shinda kwenda 15888.
0 comments:
Post a Comment