Monday, 4 December 2017

DRC CONGO: Zaidi ya watu 12,000 waikimbia nchi hiyo kutokana na machafuko

Zaidi ya watu 12,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekimbilia nchi jirani ya Zambia kutafuta hifadhi kutokana na machafuko Kusini Mashariki mwa nchi yao.

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa, hali ya wakimbizi hao ni mbaya, na wanakosa mahitaji muhimu kwa sababu ya uhaba wa fedha lakini pia kuondelea kuongezeka kwa wakimbizi hao ambapo UNHCR inasema inahitaji Dola za Marekani Milioni 236 Kuwasaidia wakimbizi hao.
Tangu mwezi Agosti pekee, zaidi ya wakimbi 8,000 wameingia nchini Zambia wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Mdororo wa usalama nchini DRC umesababisha raia wengi kuyahama makazi yao ambapo hayo yanajiri wakati ambapo chama kikuu cha upinzani nchini DRC, UDPS kikidai kwamba hakimtambui Waziri Mkuu Bruno Tshibala kama mwanachama na kiongozi ndani ya chama hicho.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top