Sunday, 24 December 2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa:sasa ni mwisho mkiendelea tutawafukuza

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kuachana na makundi yanayoigawa Manispaa hiyo kwani yanakwamisha utekelezaji wa miradi
Tokeo la picha la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa


Waziri mkuu wakati akiwa katika ziara yake ya siku moja mkoa wa Ruvuma wakati akizungmza na watumishi pamoja na Madiwani hao ambapo amewaambia kama watashindwa kuzimaliza tofauti zao yeye atawafukuza.

“Madiwani mnaigawa Halmashauri, pamoja na nguvu mliyonayo ya kuiendesha Halmashauri lakini mnaiendesha vibaya, miradi haijengwi vizuri, mmeingiza maslahi binafsi, wakati mwingine pesa zinatumwa mnaanza kubishana tu, sasa ni mwisho mkiendelea tutawafukuza, amesema Waziri Mkuu.

Majaliwa ameongeza kuwa serikali inakusanya kodi ili wananchi wapate maendeleo lakini wao wanachelewesha miradi ya maendeleo kwa malengo ya kuikwamisha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo hatakubali na atawafukuza.

Aidha amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kwa kazi nzuri anayoifanya na kumtaka kuripoti kwake endapo pesa zitaingia kisha Madiwani kuanza kubishana bila utekelezaji ili awashughulikie hata kama ni Meya wa Manispaa hiyo.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © MOtown TV | Designed With By Blogger Templates
Scroll To Top