Aliyewahi kuwa Mr University mwaka 2002 Tanzania, Matukio Chuma Ijumaa hii amerudi nchini na kupokewa na umati wa mashabiki katika Uwanja wa JK Nyerere Airport akitokea nchini Marekani alipokuwa akifanya shughuli zake za masomo.
.
.
Akiongea na waandishi wa habari mapema Jana muda mchache baada ya kuwasili, Chuma amesema akiwa nje ya nchi amejifunza kuthubutu pamoja na kutafuta fursa kwaajili ya Watanzania wenzake.
“Namshukuru mungu sana nimeweza kufanikisha wengi katika maisha yangu, hii haikuwa safari ya masomo ilikuwa safari ambayo imezalisha vitu vingi sana katika maisha yangu,” alisema Chuma.
Aliongeza, “Pia safari yangu imekuwa na mafanikio mengi kwa Watanzania ingawa wengi walikuwa hawachangamkii fursa, nimetoa fursa nyingi sana kupitia mitandao lakini Watanzania hawazichangamkii, tunajiweka nyuma sana kwenye mambo mengi,”
Msomi huyo aliweza kulakiwa na mastaa mbalimbali wa filamu wakiwemo Bella Fasta, Baby Madaha pamoja na msanii wa BongoFleva, Z Anto.

0 comments:
Post a Comment