Mifuko kibao ya mawe kwa gramu ya dhahabu
Mchimbaji hupitia njia nyembamba, wakati mwenzake akimsubiri. Mifuko ya mawe ambayo husongamana kuelekea upande wa kuingilia machimboni, huwa iko mbele yake. Ukiachana na kilimo, machimbo ya Artisanal ni muhimu zaidi kwa maisha ya binaadamu katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC.
Kilo 30 kwa mzigo mmoja
Wabeba magunia ya michanga huipeleka kiwandani kwa ajili ya kusafishwa. Hulipwa Franc za Kongo 500, ambayo ni sawa na Euro 0.29, kwa kiwango cha sasa cha kubadilisha fedha Mashariki mwa Kongo kwa gunia moja na wanaweza kutengeneza kiasi cha pesa kwa siku. Ni miongoni mwa wanaopata kiasi kidogo zaidi cha fedha kwenye machimbo, na katika machimbo haya mara nyingi ni wale walitokea maeneo mengine.
Kufunikwa kwenye miamba
Mtu huyu amepiga magoti mbele ya mwamba huku akipasua mawe ya dhahabu kwa kutumia jiwe la kupasulia. Baadae mawe yanayobaki huvunjwa kwa njia ya kawaida katikati ya miamba ili kupata dhahabu. Njia hii huchukua muda mrefu; inaweza kuchukua masaa kadhaa kulishughulikia basini moja la plastiki. Wabebaji wa maji na mawe ya dhahabu huonekana wakipanda na kushuka kwenye machimbo.
Udongo wa thamani
Huyu anamimina udongo wenye dhahabu kwenye mtaro wenye kifaa cha kudhibiti kasi. Madini safi ambayo huletwa na wataalamu wa kifaa hicho huchanganywa na maji na kumwagwa kwenye mtaro wenye udongo. Kutokana na uzito mkubwa, mawe ya dhahabu yanayosalia huganda kwenye blanketi lililokwa mtaroni, wakati masalia humwagikia chini. Mawe hukusanywa na kuchujwa kwenye beseni la plastiki kwa kutumia mekyuri.
Mauzo ya awali
Mfanyabiashara kutoka machimbo hayo anakagua kiasi gani atakitoa kwa dhahabu aliyoletewa. Dhahabu na madino ya mekyuri yanayoonekana kwenye ndoo ya plastiki ya muuzaji yakiwa na rangi ya chuma na kijivu kabla ya kusafishwa kiwandani. Wachimbaji wengi hutarajia kuuza kiwango kidogo cha dhahabu kwa wafanyabiashara wa eneo la machimbo.
Kuisafisha dhahabu
Wafanyabiashara wakubwa huunguza dhahabu na acidi ya Nitric kwenye moto mkali ili kuondoa masalia yote. Wafanyabiashara hao hushughulika na kiwango kikubwa sana cha dhahabu kuliko wafanyabiashara wa ndani. Mara nyingi huuza nyingi zaidi kwa wiki. Ziada ya faida yao ni ndogo kuliko wafanyabiashara wa ndani, ingawa huuza kwa kiasi kikubwa, na kujihakikishia kipato kikubwa.
Poda ya thamani
Baada ya kuichoma, dhahabu inapimwa kwenye mzani wa umeme. Katika hatua hii, dhahabu huwa imefikia kati ya asilimia 92 hadi 98 ya uhalisia wake, kwa kutegemea asili yake.
Uyeyushwaji wa dhahabu
Baada ya kuyeyushwa, dhahabu huwekwa kwenye chombo cha kutengenezea umbo. Chombo hicho kikishatolewa kwenye moto mkali wa tanuru, mchimbaji kwenye eneo la kuyeyusha humimina dhahabu iliyoyeyuka kwenye kaboni nyeusi ama grafiti kwa ajili ya kutengenezwa umbo. Ndani ya tanuru, dhahabu hufikia kipimo cha joto la digrii 1,500, Celcius. Huchukua takriban dakika 20 kuyeyusha kilo kadhaa za dhahabu.
Kipindi cha kupoozwa
Dhahabu ambayo tayari imeundwa hutolewa kwenye chombo na kuwekwa na wachimbaji kwenye kwenye eneo la wazi na wakati huo bado hutoa mvuke wa moto.
0 comments:
Post a Comment